Deogratius Mongela na Chande Abdallah
SIKU chache
baada ya kuvunjika kwa ndoa ya Khadija Shaibu ‘Dida’, aliyekuwa mumewe,
Mtangazaji wa TV1, Ezden Jumanne ameibuka na kutoa sababu kuu tatu za
kutengena kwao, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.
Akizungumza
na waandishi wetu katika nyumba aliyohamia kwa sasa, Kijitonyama, Dar,
Ezden alisema mgogoro kati yake na Dida ulianza zamani ambapo Dida
alikuwa na tabia ya kurudi usiku mnene, Ezden alidai kadiri siku
zilivyozidi kusonga mbele, tabia hiyo ilizidi kuonekana ingawa alikuwa
akimuonya mara kwa mara.
BIG BROTHER NDIYO TATIZO
Pamoja na sababu hizo, Ezden aliitaja sababu kuu iliyoanza kuzua
mgogoro uliosababisha kuvunjika kwa ndoa hiyo ni Shindano la Big Brother
Africa linalotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Alisema
siku moja mtalaka wake huyo alimweleza kuwa kuna rafiki yake aliyemtaja
kwa jina la Furaha amempa mchongo wa kuwa mgeni staa (celebrity guest)
ndani ya Jumba la Big Brother na kumuomba ampe ridhaa ya kwenda huko.Akizidi kumwaga data mbele ya kinasa sauti cha Risasi Mchanganyiko, Ezden alisema:
“Nilimruhusu
kwa moyo mmoja ambapo pia aliniomba nimsaidie kumpa uzoefu juu ya lugha
ya Kiingereza ili akaendane na kanuni za Big Brother.
“Kama mume
nilimsapoti kwa nguvu zote, siku nyingine kama nikiwa nimerudi nyumbani
mapema mimi mwenyewe nilikuwa nikimfundisha ‘tense’ mbalimbali.”
Katika aya nyingine, Ezden alisema kuna siku Dida alimfungukia kuwa
hatakwenda Big Brother kama mgeni staa kwani anatakiwa kuingia kama
mshiriki na kumwambia kuwa alikuwa akiogopa kumwambia ukweli mapema.
“Nilimkatalia
ndipo alipocharuka, huwezi amini alifikia hatua ya kusema nambania
zali lake. Niliumia sana siku ile ikabidi nimuulize kama anaithamini Big
Brother kuliko ndoa yake, hakunijibu.
“Kama mume ilibidi niwaulize wazazi na mashemeji zangu kama
wamemruhusu Dida kushiriki shindano hilo kama alivyoniambia, walidai
aliwaambia kuwa mimi ndiye niliyemruhusu ndiyo maana nao hawakuwa na
pingamizi.
“Baada ya kuwaelewesha waliniambia hawakupenda mambo hayo ya Big Brother kwa kuwa yana udhalilishaji ndani yake,” alisema Ezden.
Siku ya tukio, Ezden alisema alikuwa akioga bafuni na simu yake
ilikuwa kitandani, ghafla Dida alimfuata na kumuuliza kwa nini aliweka
password!
“Alipiga
kelele mpaka majirani wakaanza kujaa nyumbani kisa ‘password’
niliyoiweka kwenye simu yangu. Nikamuuliza yeye si ndiye aliyesema kuwa
kila mtu awe na simu yake! Akaanza kunipa maneno ya kejeli.
“Hapo nikaona heshima yangu inashuka. Kiukweli nilimpiga mpaka
nikamuumiza. Baadaye akaondoka kwa hasira kumbe alikwenda kuwachukua
ndugu zake.
“Walipokuja
tukajitahidi kusuluhisha lakini kila nilipopewa nafasi ya kuzungumza,
Dida aliniingilia. Kwa kuwa tulishawahi kukaa vikao vingi sana kabla
lakini hakuna tulichoweza kusuluhisha, niliona hakuna haja ya kuendelea
naye,” alisema Ezden na kuongeza kuwa kikao hicho kiliisha kwa ahadi
kwamba angetoa talaka kwa Dida ambaye naye alionekana kuikubali.
Ezden
alisema, Juni 28, mwaka huu alimpa Dida talaka tatu na kuongeza kuwa
hategemei kurudiana naye wala kuoa hivi karibuni.Kwa upande wake, Dida
alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema: “Mimi sina la kusema na wala
sitaki kulumbana na mtu.”>>>>GPL
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro






Post a Comment
Post a Comment