Shughuli za uokozi zikiendelea baada ya ndege ya mizigo kuanguka jijini Nairobi
Watu wanne akiwemo Rubani wa
ndege moja ya mizigo, wamefariki dunia baada ya ndege walimokuwa
kuanguka mapema leo asubuhi katika mtaa wa Embakasi jijini Nairobi.
Kwa mjibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini
Kenya, ndege hiyo ilianguka dakika chache tu baada ya kuruka kutoka
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.Ndege hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba shehena ya Miraa ama Mairungi kuelekea Mogadishu nchini Somalia.
Uchunguzi umeonyesha kuwa ndege hiyo huenda iligonga mlingoti wa stima karibu na mtaa wa Embakasi, mjini Nairobi na kuanguka.
>>>>BBC
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro






Post a Comment
Post a Comment