Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi kwenye
Viwanja vya Kibanda Maiti, mjini Zanzibar, Mei 4, 2014 kueleza kwa nini
CCM inawataka Watanzania kuiunga mkono kuhusu msimamo wake wa kutaka
Tanzania iendelee kuwa katika mfumo wa serikali mbili ndani ya Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar baada ya mchakato wa Katiba mpya.
Mjane wa Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, Mama Fatuma Karume akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshukuru na kumpongeza Mama Fatuma Katume kwa hotuba nzuri 'iliyoshiba'.
Ni
serikali mbili tu: Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye,
akionyesha alama inayotumiwa na chama chake kujinasibu kuwa kinahitaji
serikali mbili katika katiba mpya, alipohutubia wananchi katika mkutano
huo wa Kibanda maiti, Mei 4, 2014 mjini Zanzibar.
Kada machacahari wa CCM kutoka Zanzibar, Asha Bakari Machano akihutubia mkutano huo wa Kibanda maiti, Mei 4, 2014.
Kada
mwingine ambaye pia ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alitema
cheche kwenye mkutano huo, wakati akieleza kwa nini CCM inaona kwamba
mfumo wa serikali mbili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo
unafaa.
Wananchi
wakishangilia huku wakionyesha kuunga mkono msimamo wa CCM wa kutaka
mfumo wa serikali mbili katika katiba mpya, wakati wa mkutano huo.
Post a Comment
Post a Comment