Mtu
mmoja kati ya wanne waliolipukiwa na mabomu, Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini
Unguja, amefariki dunia na kuzikwa jana Visiwani Zanzibar. Marehemu
aliyetajwa kwa jina la Juma Abdallah Juma (32), alifariki dunia kutokana
na majeraha makubwa aliyopata sehemu mbalimbali mwilini.Katibu
wa Hospitali ya Mnazi Moja, Hassan Makame alisema marehemu alifariki
juzi jioni wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo.Alisema
majeruhi, Pandu Haji Pandu aliyekatika mguu amehamishiwa katika Chumba
Maalumu (ICU) kutokana na majeraha makubwa aliyopata.Majeruhi
mwingine ni Shaaban Khamis Ibrahim ambaye anaendelea kupatiwa matibabu
ikiwa ni pamoja na kutolewa kitu kigumu sehemu ya kiunoni
kilichosababishwa na mlipuko huo.Makame alisema majeruhi Simai Hussein Hassan alipatiwa matibabu na kuruhusiwa baada ya hali yake kuimarika.Akizungumza na gazeti hili katika wodi ya upasuaji wa mifupa
Hospitali
ya Mnazi Mmoja, majeruhi Shaaban Khamis Ibrahim, alisema mkasa huo
ulimpata wakati alipokwenda karibu na karakana ya uchongaji vyuma baada
ya pikipiki yake kupata matatizo.“Baada
ya kazi zangu za uvuvi, niligundua pikipiki yangu ina matatizo,
nikaenda gereji kuifanyia matengenezo na nilipofika jirani na wachonga
vyuma, nikasikia mlipuko na kitu kizito kilikuja kunipiga kiunoni,”
alisema majeruhi huyo.Alisema madaktari walimtoa chembechembe za mabaki ya vitu mwilini, ingawa anatakiwa kufanyiwa vipimo zaidi.Akizungumza
na gazeti hili jana, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame
alisema mtu mmoja anashikiliwa na polisi kuhusiana na matukio ya
milipuko yaliojitokeza katika maeneo matatu Zanzibar.Askofu
wa Kanisa la Anglikana Zanzibar, Michael Hafidh alisema vyombo vya dola
vinatakiwa kuwaeleza wananchi mhusika wa vitendo vya hujuma dhidi ya
makanisa Zanzibar.
-Mwananchi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro






Post a Comment
Post a Comment