Akizungumza
nyumbani kwake eneo hilo, Dar es Salaam jana, baba wa mtoto huyo, Salum
Ally alikanusha mtoto huyo kuwa mwanafunzi katika madrasa ya mtuhumiwa.
Ally
alisema siku ya tukio akiwa anarudi kazini saa 11 jioni, alipopita eneo
hilo la madrasa aliona umati wa watu umezunguka eneo hilo na alishangaa
kabla ya kuendelea na safari yake.
Alisema
baada ya kufika jirani na nyumbani kwake, alipishana na mkewe akilia
huku akikimbilia eneo la tukio, akipiga kelele kuwa mtoto wao Jamal
kachinjwa.
Mama
wa marehemu, Halima Selemani alisema siku ya tukio, marehemu baada ya
kujaladia madaftari yake na mwenzake aitwaye Ramadhani waliondoka
akimtaka amsindikize kwa mjomba wake eneo la jirani na hapo akachukue
kalamu.
Alisema
rafiki yake alimhimiza mwenzake waondoke, huku yeye akiwa ametangulia
ndipo mwalimu huyo alipomshika mkono marehemu na kuingia nae ndani na
mwenzake alirudi na kukuta ameshikwa mkono na ndipo alipoanza kumsihi
amwachie.
“Alimsihi
sana amwachie kwani hajui kosa lake, lakini mwalimu huyo hakumsikiliza
badala yake akaanza kumchoma kwa kisu machoni na usoni,” alisema.
Mtoto huyo alizidi kumwombea mwenzake, lakini akiwa hajui lolote alimshuhudia mwalimu huyo akimchinja mwenzake.
Mwili
wa mtoto huyo ulizikwa juzi makaburi ya kwa Mbiku, wakati mwalimu huyo
akizikwa kwao Kisiju Pwani. Baadhi ya majirani walidai ndugu za marehemu
waliwasilisha cheti polisi mwaka 2007 kuwa aliugua ugonjwa wa akili.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema alifika nyumbani kwa marehemu Jamal
na kuwataka ndugu kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi
na kuiasa jamii kutowaficha watu ambao wana matatizo hususan yale ya
akili.
-Mwananchi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro






Post a Comment
Post a Comment