Home
»
Matukio
» Watu 79 Watiwa Mbaroni Kwa Kuishi Nchini Bila Vibali na Kufanya Kazi Zinazoweza Kufanywa Na Watanzania
WATU 79 wamekamatwa na Idara ya Uhamiaji nchini kwa kosa la kuishi nchini bila vibali na kufanya kazi wasizo na taaluma nazo.
Naibu Kamishna wa Uhamiaji Dar es Salaam, John Msumule jana alisema watuhumiwa hao wanatoka katika nchi 15.
Nchi hizo na idadi ya wahamiaji haramu ni Nigeria (4), China (20), Ethiopia (23), Korea (9), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC (6), Somalia (3),Uganda (2), Madagascar (5), Burundi (2), Ivory Coast (1), Lebanon (1), India (1), Zimbabwe (1) na Ghana (1).
Alisema katika ‘kamata kamata’ hiyo pia wamefanikiwa kukamata Watanzania watatu, ambao wamekuwa wakijishughulisha na kukusanya, kuwahifadhi na kuwasafirisha wasichana kuwapeleka nchi za mbali, kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali.
“Tumewakamata wasichana sita ambao walikuwa wamekusanywa na watanzania hao ili kusafirishwa na tutawachukulia hatua za kisheria ili kutoa fundisho kwa wengine wenye nia ya kufanya mtindo kama huu,”alisema Msumule.
Aliongeza kuwa idara hiyo imewarudisha nchini mwao wahamiaji 23 raia wa Ethiopia na watuhumiwa nane wa nchi mbalimbali,wamefikishwa mahakamani. Alisema shughuli ya kuwarejesha raia wengine katika nchi zao zinaendelea.
Msumule aliwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni na nyumba za kupanga, wahakikishe wanatambua wateja wao ni raia wa wapi na anafanya kazi gani, kabla ya kufanya naye mkataba wa aina yoyote.
Aliwataka pia watanzania wanaooa na kuolewa, wahakikishe wanafahamiana na mtu huyo na kumchunguza kujua anakotoka na yupo nchini kwa kazi gani, la sivyo mtu akibainika anaishi na mhamiaji, anaweza kujiingiza katika matatizo.
“Sisi hatutajali, tutamkamata kwa kosa la kumhifadhi kwa hiyo lazima wajenge dhana ya kuwachunguza watu hao, hata wasichana wa kazi za ndani, lazima umjue vizuri na sio unamchukua tu bila kujua historia yake ,” alisema.
Msumule aliwataka raia wengine ambao hawana vibali vya kuishi nchini, waondoke wenyewe na wasisubiri hadi sheria ichukue mkondo wake.
“Wapo wengi, tunachoomba waondoke wenyewe bila kushurutishwa,wengine wanafanya kazi ambazo hata watanzania wanaweza kuzifanya, wakubali na waondoke,” aliagiza.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment