Home
Β»
Matukio
Β» Mtu Mmoja Afariki Dunia na Wengine 4 Wamejeruhiwa katika ajali ya basi La Mohammed Trans Iliyotokea Mlima Sekenke Singida
BASI la kampuni ya Mohammed Trans aina ya scania T.858.AWY lililokuwa likitokea jijini Mwanza likielekea jijini Dar-es-salaam,juzi lilipata ajali na kusababisha kifo cha utingo wake na kujeruhi vibaya abiria wanne.
Utingo huyo aliyefia hospitali ya wilaya ya Iramba akipatiwa matibabu,ni Abdallah Athuman (35) mkazi wa Shinyanga mjini.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida, ACP Simon Haule, alisema ajali hiyo imetokea Januari 9 mwaka huu saa 6.45 mchana huko katika mlima Sekenke wilaya ya Iramba.
Alisema siku ya tukio basi hilo lililokuwa likiendeshwa na Jovin Jonson (35) lilipofika eneo la tukio,liligonga kingo za daraja na kusababisha kifo cha utingo na abiria wengine wanne kujeruhiwa.
Haule alitaja waliojeruhiwa kuwa ni mkazi wa Kahama mkoani Shinyanga Asha Said (20) mkaguzi wa ndani wa mahesabu wa kampuni ya Mohammed ambaye amekatika mguu wa kushoto.
βMkulima na mkazi wa Tengo wilaya ya Kahama,Lucas Deo (22) amevunjika miguu yote miwili na wote wawili na mwenzake Asha,wamehamishiwa hospitali ya rufaa Bungando jijini Mwanza kwa matibabu zaidiβ,alisema kaimu kamanda huyo.
Haule allisema Felix Matimati (30) mkazi wa Shinyanga mjini,yeye ameteguka mguu wa kushoto na amepatiwa matibabu ya kuruhusiwa,wakati Alafati Said (24) mkazi wa jijini Mwanza,amepata majeraha mguu wa kushoto,ametibiwa na kuruhusiwa.
Kaimu kamanda huyo,alisema chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya usukani wa basi hilo na hivyo kupelekea dereva Jovin kushindwa kulimudu.Dereva huyo hivi sasa anashikiliwa na polisi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment