Home
»
michezo
» Mmbwana Ally Samatta Anyakua Tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika Anayechezea Barani Afrika
Mwanasoka raia wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mmbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika, wakati tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika ikienda kwa Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kabumbumbu katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku kuamkia leo mjini Abuja nchini Nigeria.
Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya Cameroon. Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Ivory Coast.
Kocha bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Cote d’Ivore ambayo inashinda kwa mwaka wa pili mfululizo wakati Klabu bora ya soka barani Afrika ni – TP Mezembe, kutoka DR Congo ambapo mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon na Mwamuzi bora wa mwaka ni – Bakary Gassama kutoka nchini Gambia.
Tuzo hizo zilipambwa na shamra shamra za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu pamoja na wanenguaji walitumbuiza akiwemo mwanamuziki nguli kutoka nchini Mali, Salif Keita pamoja na mwanamuziki kutoka Nigeria Omowumi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Ujumbe wa Samatta kwa Waliotamani Genk Ingepangwa Kundi Moja na Man United28 Aug 20160
Mchana wa August 26 2016 shirikisho la soka barani Ulaya UEFA lilichezesha droo ya kupanga makund...Read more ?
- Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya mwanasoka bora Ulaya26 Aug 20160
Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mwanasoka bora Ulaya. Ron...Read more ?
- Makundi ya klabu Bingwa Ulaya 2016/201726 Aug 20160
Droo ya kupanga Makundi ya klabu Bingwa Ulaya 2016/2017 ratiba kamili ya hatua ya makundi ya Uefa ...Read more ?
- MICHEZO Bilionea anayetaka kuinunua Simba, ametaja kilichomsikitisha katika mkutano wa Simba01 Aug 20160
Siku moja baada ya mkutano mkuu wa Simba kufanyika na kukubali kupitisha maadhimio ya mabadilik...Read more ?
- Gonzalo asajiliwa na Juventus kwa pauni milioni 7528 Jul 20160
Klabu ya Juventus wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Argentina, Gonzalo Higuain kutoka klabu...Read more ?
- Hongera Yanga kwa mlipofika, tujipange upya28 Jul 20160
Ni muda mrefu soka la Tanzania kwenye ngazi za vilabu limeonekana kuzorota kufuatia vilabu vyake k...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment