Picha: Kitale (Kushoto) akiwana mtangazaji Salma Msangi bamoja na Stan Bakora
Msanii wa filamu na vichekesho, Musa Kitale jioni ya leo (jana) akizungumza kwenye studio za Magic FM,kipindi cha Afrika Kabisa kwenye kipengele cha African Movies, alisema wazi kuwa hawapendi bongo movies kwani wanapenda kurudia rudia na kukopi filamu za nje na kusisitiza hata akiziangalia filamu zao huwa haoni jipya na hazina ubunifu.
Akaendelea zaidi kufafanua kuwa yeye sio mwana bongo movies na wala hayuko karibu nao kwani anaogopa kuwaambukizwa ‘kaugonjwa’ kakukopi kopi kitu mabcho aliwahi kumutahadharisha hata alikuwa lafiki yake wa karibu marehemu Sharo Milionea.
Kitale alikuwa pamoja na Stan Bakora wakielezea ujio wa filamu ya SAFARA HASARA ambayo ndio ya mwisho ya Kitale na Sharo Milionea kurekodi pamoja.
Akielezea filamu hiyo Kitale amesema japo kuwa filamu hiyo wamerekodi mwaka 2012 lakini hadi sasa hakuna hata filamu moja ya kibongo ambayo ina ubunifu kuifunika filamu.
Filamu ya SAFARA HARASA itaingia sokoni mwezi huu tarehe 20 mwaka huu.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment