Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
STAA aliyetikisa kwenye Bongo Fleva na single ya Maumivu Niache, Khadija Maige ‘Kadja Nito’,  ameweka wazi kuwa yupo huru baada ya kuachika na aliyekuwa mpenzi wake, hivyo nafasi ya mwenza mpya inakaribishwa ila vigezo na masharti vitazingatiwa.
Staa aliyetikisa kwenye Bongo Fleva na single ya Maumivu Niache, Khadija Maige ‘Kadja Nito’.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Kadja alisema amekuwa akiteswa sana na uhusiano wake wa kimapenzi hivyo kwa sasa ameamua kuachana na mwenza wake na yupo huru, ila atakayemhitaji kwa sasa ahakikishe anafuata taratibu na mila za Kiafrika.
“Kwa sasa nimeachika na mpenzi wangu na wala sina mpango wa kurudiana naye, hivyo kama kuna anayeniona namfaa ni vizuri sasa akafuata taratibu za Kiafrika kwa kujitokeza kwa wazazi wangu, ili waweze kumtambua kwanza na nitakuwa tayari kwa kumpokea atakayefanya hivyo,” alisema Kadja.Juzikati Kadja aliachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Siulisema ambao unafanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya radio na televisheni.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top