Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kha! RB namba KTN|RB/11213/2014 –UTAPELI inamsaka msanii wa muziki na sinema za Kibongo, Hemed Suleiman ‘PHD’ tangu mwaka jana, akidaiwa ‘kuchikichia’ nguo za shilingi laki saba, mali ya aliyekuwa Mtangazaji wa EATV,  Nasra Dattani ‘Lady Naa’ ambaye alimkabidhi begi lake la nguo baada ya kumaliza kurekodi filamu iitwayo Catherine.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Lady Naa alisema kuwa alimvumilia Hemed kwa muda mrefu kwani alimpa mzigo huo na kumuomba akaushushe dukani kwa rafiki yake maeneo ya Kinondoni lakini hakufanya hivyo na alipokuwa akimkumbusha alikuwa akimwambia kuwa atampelekea.

“Kila nikikutana naye nilikuwa namuomba anirudishie anasema nifanye lolote na kinachonishangaza amezipeleka wapi maana mle kulikuwa na nguo za kike ambazo nilizitoa Uingereza,” alisema Lady Naa.

Alidai kwamba baada ya kumzungusha kwa muda mrefu ndipo alipoamua kumfungulia kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama, Dar ambapo hadi leo anasakwa. Baada ya habari hizo kulifikia gazeti hili, mwanahabari wetu alimwendea hewani Hemed lakini namba yake haikupatikana hivyo jitihada zinaendelea.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top