March 21, 2025 09:20:37 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mwanamuziki  wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amepondwa vibaya katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Mhe. Kapt. John Komba, baada ya kuvaa kigauni kilichombana na kumuonyesha maungo yake ya mwili mbele ya viongozi mbalimbali wa Serikali akiwepo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
  
Mwanamuziki wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiimba pamoja na wasanii wenzake kwenye msiba wa Komba.
  
Baadhi ya watu waliofika katika Viwanja vya Karimjee vilivyopo Posta jijini Dar, walianza kunong’onezana baada ya mwanamuziki huyo kujitokeza mbele na kuimba kipande cha shairi lake huku wakisema kuhusu kigauni alichovaa bi’dada huyo.
 
“ Jamani hii aliyovaa si ‘tight’ kabisa, maana yupo tofauti na wenzake ambao wote wamevaa nguo za heshima zinazowasitiri  maumbo yao, kwa nini yeye ameamua kuvaa hivyo?” alisikika mama mmoja ambaye naye alikuwemo kwenye maombolezo.
 
Mwandishi  wetu alimtafuta Shilole na kumuuliza kuhusiana na hilo alisema hakuvaa vibaya isipokuwa alionekana vile kutokana na umbo la mwili wake.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
05 Mar 2015

Post a Comment

 
Top