March 24, 2025 03:28:31 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwanamziki Ommy Dimpoz ameyasema hayo leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM alipokuwa anautambulisha wimbo wake wa Wanjera ambao mrembo Wema Sepetu amecheza kama Wanjera kwenye video wa wimbo huo na kushiriki kupiga picha za kuutangaza wimbo huo.

Ommy alisema haoni kama kuna tatizo lolote kati yake na swahiba wake huyo licha ya Diamond kutoandika chochote kuhusiana na wimbo huo kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wasanii wengine.

 “Labda hajaposti yupo busy na simu yake, hata mimi kuna vitu vingine huwaga anaposti na mimi vinanipita pia,” amesema Ommy. “Kwahiyo huwezi ukasema hajaposti kwa sababu fulani na fulani. Diamond si yuko na Zari au? Kwahiyo hawezi tena akawa anafocus kwa mambo ya Wema. Wala hawezi kunimind mimi kwa sababu kamuona Wema, haiwezekani. Halafu kumbukeni shemeji yetu Zari ni mjamzito msitake kuwatia watu pressure.”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
13 Mar 2015

Post a Comment

 
Top