Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wimbi la Dada zetu/wanawake kutupa watoto wachanga na wengine kuwaua na kuwanyofoa macho bado linaendelea kujitokeza katika maeneo yetu ambapo leo kuna kuna tukio limetokea mda mfupi uliopita ambapo Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa mwezi mmoja ameokotw aakiwa ametupwa na Mama yake (hajatambulika jina mara moja) katika eneo la Mahakama ya Mwanzo Sinza 'C' Jijini Dar es Salaam (Mtoto hajafa) ila amejeruhiwa kwa kiasi kidogo usoni na mbwa waliokuwa wanaranda randa nje ya eneo hilo.

Tukio hilo limetokea jana Machi 29, 2015 saa 21:30 usiku ambapo mashuhuda wa tukio wanaeleza kuwa walikiona kichanga hicho kikiwa kimetupwa nje ya geti la nyumba namba 22 inayomilikiwa na Steven Lesika ambapo kugundulika kwa tukio hilo kumekuja baada ya ya wapita njia kusikia kichanga hicho kikilia ndipo walipoto taarifa kwa mwenye nyumba.
 Mashuda wa tukio hilo wakiwa katika harakati za kumpeleka mtoto huyo kwenye Kituo cha Polisi Mabatini
Mwenye nyumba baada ya kupewa taarifa aliripoti kwa Balozi wa eneo hilo, Lucia Kaunda. Balozi aliwaandikia barua wasamaria wema ili wampeleke kwenye Kituo cha Polisi Mabatini na kufunguliwa faili lenye namba KJN/RB/3237/015.

Wasamaria wema waliochukua jukumu la kumuokoa mtoto huyo wamepewa hati ya matibabu, maarufu kwa jina la PF3, wasamaria hao hao wameambiwa na Polisi wampeleke Hospititali ya Mwananyamala. 

Naambatanisha picha za tukio, kwa pamoja tuungane kuwapa elimu watu wanaokuwa na roho ngumu kwasababu mbalimbali ikiwemo ugumu wa maisha hali inayowapelekea kuwatupa watoto wao/kuwatekeleza.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top