Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Baba mwenye nyumba anashutumiwa kumbaka msichana wake wa kazi baada ya kumlaghai.
 
Ishu hiyo imetokea Chang’ombe DAR ambapo majirani walitishia kuandamana kwa kuwa baba huyo anashutumiwa lakini hakuna hatua yoyote ya kisheria iliyochukuliwa.
 
Majirani wamesema kuwa binti huyo aliwafuata akiwa analia na kulalamika kuwa tumbo linamuuma kutokana na baba huyo kumlaghai na kisha kumbaka, wakaamua kumpeleka Polisi ambako walipewa PF3 na kumpeleka katika Hospitali ya Temeke ambako alilazwa.
 
Mwenyekiti wa eneo hilo amesema alipata taarifa baada ya mke wa baba anayetuhumiwa kwenda Hospitali kumchukua binti huyo lakini walimkatalia na kumtaka aende na barua kutoka ofisi za Serikali.
 
Daktari aliyemfanyia uchunguzi amesema hakuna dalili ya msichana huyo kuingiliwa, majirani hao wameamua kumpeleka ofisi za ustawi wa jamii ili wafanye uchunguzi zaidi.
 
Mke wa mwanaume huyo amesema alipigiwa simu na mpangaji mwenzake akimpa taarifa hizo lakini alipomuuliza mume wake  alikataa kufanya kitendo hicho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top