Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mshambulizi wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameweka wazi kuwa ataachana na mabingwa mara nne wa kihistoria wa Afrika, TP Mazembe mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake. Akizungumza na mwandishi wa mtandao wa www.shaffihdauda.co.tz muda mfupi uliopita mshambulizi huyo wa Taifa Stars amesema kuwa hana furaha katika timu hiyo ya Congo.

  Samatta ambaye alipata nafasi ya kufanya majaribio katika klabu ya CSKA Moscow ya Urusi mwezi uliopita amepewa ofa nyingi barani ulaya na kama ataendelea kuchezea TP basi atakuwa ni mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi barani Afrika. Hivi karibuni kuna vyombo vya habari ambavyo viliripoti kuwa mchezaji huyo ana furaha kuendelea kuichezea TP lakini amesema huo ni uzushi mkubwa.

 ” Sina furaha hapa ( TP Mazembe) nitaondoka wakati wa majira ya usajili katikati ya mwaka na sitaongeza mkataba” anasema Samatta. 


Source:shaffihdauda.co.tz... 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top