Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mchezaji mganda alieleta vuta nikuvute kati ya Klabu Vigogo Nchini baada ya kuhama kwenda nyingine kwa mizengwe mikubwa, Emmanuel Okwi, Leo hii alileta raha kubwa kwa Simba baada ya kufunga Bao pekee na la ushindi walipoilaza Yanga Bao 1-0 kwenye Mechi ya Ligi  Kuu Vodacom.
Bao hilo la Okwi lilifungwa Dakika ya 53 na kuipandisha Simba hadi Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 26 kwa Mechi 17 na juu yao wapo Mabingwa Watetezi Azam FC wenye Pointi 30 kwa Mechi 16 na Yanga bado wapo kileleni wakiwa na Pointi 31 kwa Mechi 16.
Yanga walimaliza Mechi hii wakibaki Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Haruna Niyonzima kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu karibuni na mwisho.
MATOKEO- Mechi zilizopita:
Jumamosi Machi 7
Coastal Union 2 Kagera Sugar 2  
JKT Ruvu 0 Azam FC 1

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top