Home
»
Udaku
» Kimini cha Trafiki Chazua Balaa, Raia Waacha Kazi Zao na Kuanza Kujadili Kivazi Hicho
Kimini alichovaa trafiki wa kike ambaye jina lake halikupatikana mara moja, kinadaiwa kuzua balaa huku wahuni wakimpigia miluzi.
Tukio hilo lililojaza kadamnasi na kushuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri wiki iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar, majira ya asubuhi.Bila kujua ‘amefotolewa’ trafiki huyo alikuwa amesimama pembeni akimtazama mwenzake wa kiume aliyekuwa akiongoza magari huku kimini chake cha sare ya kazi kikiwa kimepanda juu na kuonesha sehemu ya upaja wake wa haja.
“Jamani mbona majanga? Waone wahuni wanavyokitolea macho kimini cha trafiki na hapo amesimama. Akiinama kidogo tu mambo yote hadharani,” alisema mama aliyekuwa akiwashangaa raia walioacha kazi zao na kujadili kivazi hicho cha trafiki huyo.
“Tunachojua ni kwamba hizi sare huwa wanashonewa na serikali siyo kwamba wanashona wenyewe. Kazi yao inahitaji kufuata maadili kwa kuwa ni watumishi wa umma. “Itakuwa ameongezeka mwili kwa sababu mbali na kuwa kifupi pia kinambana kama kile cha trafiki mrembo wa nchini Kenya aliyeibua gumzo mwaka jana.
“Au inawezekana washonaji hawakumpima vizuri kwa sababu sketi zao zinatakiwa zifike chini ya magoti,” alisema jamaa mmoja aliyekuwa akijaribu kutafuta majibu ya kimini hicho.
Ili kupata mzani wa habari hiyo kuhusu mavazi ya trafiki wa kike hasa urefu wa sketi za trafiki wa kike, gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga lakini alipopigiwa simu, iliita mara kadhaa pasipo kupokelewa.
Kupata story zingine zaidi kuwa nasi karibu kwa ku bonyeza {HAPA}
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- VIDEO: Mama Wema Aeleza Beef yake na Man Fongo Kisa……..09 Sep 20160
NI Mama Wema Sepetu ambae ameingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kutofautiana na mkali wa ...Read more ?
- Busu la Nelly Kamwelu shavuni kwa Diamond akiwa na Wizkid lawatoa povu mashabiki (Video)25 Aug 20160
Haipiti wiki bila Diamond kuwatoa povu mashabiki, hata kama alichokifanya si kwamba alidhamiria...Read more ?
- Picha za Masanja na Mke wake Zazua Maswali Kwa Mashabiki wake..Wadai Mke wa Mchungaji Apaswi Kuvaa Hivyo19 Aug 20160
Baada ya Harusi ya Mchekeshaji Masanja na Mkewe iliyofungwa Jumapili iliyopita wawili hao wameon...Read more ?
- AUDIO: Kitu Diamond kasema kuhusu yeye kuwa mapenzini na Hamisa Mobetto03 Aug 20160
Ukaribu wako kwenye mitandao ya kijamii siku za karibuni unaweza kuwa ulikukutanisha na stori...Read more ?
- Shamsa Ford Amuweka Wazi Mpenzi wake Mpya03 Aug 20160
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa baada ya kuachana na mpenzi wake wa...Read more ?
- Madai: Flora Amwangukia Mbasha30 Jul 20160
Habari ya mjini ni Mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha kudaiwa kumwangukia mumewe waliyetengana, Em...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment