Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwanamuziki wa bongo flavor ajulikanaye kama Ney wa Mitego ametangaza kuwa baada ya kujipatia watoto watatu, hana tena mapenzi na mama watoto hao bali ana mapenzi na watoto hao.

Kwa kauli hiyo, ni sawa na mama watoto hao kuchukuliwa kama bahasha maana bahasha ikishafikisha barua, inakuwa haina umuhimu tena bali kinachofanyiwa kazi ni barua iliyokuwa ndani.

Binafsi kama mwanaume sikufurahishwa na kauli kama hii kwamba hataki mazoea na mwanamke bali mapenzi ni kwa watoto, na je kama si huyo mwanamama hao watoto angeweza kuwazaa mwenyewe.

Huu pia ni ujumbe kwa wale wenye tabia kama za huyu jamaa na pia wale wanaotelekeza mama na watoto wanaenda kutafuta mwanamke mwingine.

Mtoto anahitaji malezi ya wazazi wote labda itokee bahati mbaya mmojawapo kafariki lakini unakuta mtoto anateseka, pimbi anadunda mtaani.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
18 Mar 2015

Post a Comment

 
Top