Askari polisi wawili waliokuwa katika kizuizi cha barabara katika kijiji cha
Kipara mpakani mwa wilaya ya mkuranga mkoani pwani wameuawa kwa kupigwa
Risasi huku askari mmoja akijeruhiwa baada ya kupigwa risasi kwenye paja na
Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi na kisha kupora bunduki moja.
Tukio hilo linadaiwa lilitokea tarehe 30 march 2015 majira ya saa moja usiku
Katika kizuizi kilichopo katika kijiji cha kipara wilaya ya mkuranga mkoani
Pwani sehemu inayotenganisha mkoa wa pwani na Dar es salaam ambapo watu
Wasiojulikana wakidaiwa kuwa na panga walivamia ghafla askari hao waliokuwa
Katika lindo na kuwauwa askari wawili kwa kuwapiga risasi huku askari mmoja
Akijeruhiwa kwa kupigwa risasi katika sehemu ya paja.
Licha ya ITV kufika katika kituo kikuu cha polisi kati jijini Dar es salaam
Ili kuzungumza na kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleman
Kova kuhusu tukio hilo la askari wa kanda yake,kamishana kova alikataa
Kuzungumza huku akisema anayetakiwa kuzungumza ni kamanda wa polisi mkoa wa
Pwani Urlich Matei ambaye licha ya kudaiwa kuwepo hapa jijini Dar es salaam
Na kupigiwa simu na mwandishi wa ITV lakini alipomaliza kutaja jina lake tu
Alikata simu na kisha kutuma ujumbe wa sms kwamba atafutwe kamanda wa polisi
Mkoa wa temeke ambapo licha ya ITV kufika temeke na kukuta kamanda wa mkoa huo
Hayupo na kuomba kuzungumza na kamishna Simon Siro lakini naye akakataa
Kuzunguimzia tuki hilo.
ITV ilifika katika hospitali ya temeke alipolazwa askari aliyejeruhiwa kwa
Kupigwa risasi kwenye paja na kuzungumza na mganga mfawidhi wa hospitali hiyo
Dk.Amani Malima ambaye alikiri kumpokea askari huyo huku askari huyo
Sajent Ally Jumamne kutoka kituo cha mbagala akisema anaendelea vyema kwa
Sasa.
Miili ya askari wawili waliojulikana kwa majina ya Sajent Francis na Coplo
Michael waliopoteza maisha katika tukio hilo zinadaiwa kuhifadhiwa katika
Hospitali ya taifa ya muhimbili jijini dar es salaam.
CHANZO:ITV
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment