Olvier Giroud na Aaron Ramsey walikuwa mashujaa siku ya jana kwa kuisaidia timu yao ya Arsenal kumaliza safari yao kwenye ligi wakiwa na ushindi mezani.
Arsenal walikuwa wakipambana na timu ya AS Monaco na Arsenal wakaibuka na ushidni wa mabao 2-0.

Ushindi huo hauna matunda yoyote kwa Arsenal, wametolewa kwenye Ligi ya Mabigwa Ulaya ambapo ligi hiyo imefikia hatua ya robo.
Nyumbani kwao Arsenal walifungwa 3-1 wakiwa Uwanja wa Emirates, hivyo ushindi wa jana haukutosha kuwafanya waendelee na safari ya ligi hiyo.
Wachambuzi wa soka wanasema japo Monaco wamesogea hatua moja kubwa mbele kwenye ligi hiyo, mchezo wao haukuwa kwenye kiwango kizuri japo walikinga kifua kwa nguvu zote kuhakikisha Arsenal haiwafungi zaidi ya goli 2.

Arda Turan akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza kwenye mechi hiyo
Nayo Atletico Madrid iliweza kutinga robo fainali baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 3-2 dhidi ya Bayer Leverkusen.
Timuu hizo zilitoka sare ya 1-1 pamoja na matokeo yaliyopita na hivyo kuingia hatua ya penati baada ya dakika 120 kumalizika bila kupata mshindi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment