March 23, 2025 12:32:41 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkazi wa Nyakato wilayani Kahama mkoani Shinyanga Elias Charles(30) amekutwa amejinyonga nyuma ya mlango nyumbani kwake kwa kile kinachodaiwa kukwepa deni alilokuwa akidaiwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema tikio hilo limetokea juzi asubuhi, na kwamba Charles amejinyonga kwa kile kinachodaiwa kukwepa deni la shilingi laki 1 na nusu alilokuwa akidaiwa na ndugu zake.

Akifafanua tukio hilo Kamugisha amesema mke wa marehemu Regina William(30) alitoka kwenda kuoga na aliporudi akamkuta mumewe amejinyonga nyuma ya mlango wa nyumba yao kwa kutumia kamba ya Manila.

Kamugisha amesema Uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na mke wa marehemu, umedai Elias amejinyonga kutokana na deni alilokuwa akidaiwa na ndugu zake tangu mwaka jana na si ugomvi na mkewe kama inavyodhaniwa.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya Kahama, huku jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
15 Mar 2015

Post a Comment

 
Top