Home
»
Matukio
» Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Aua Mwanafunzi Mwenzake Darasani Wakati Wakigombania Daftari la Notes
Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Ilola iliyopo katika wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga Veronica Venance(12) amefariki dunia kwa kupigwa na mwanafunzi mwenzake wakati wakigombania daftari darasani kwa ajili ya kuandika dondoo (notes).
Tukio hilo limetokea Februari 24 ,mwaka huu saa 7 na nusu mchana katika darasa la tano shule ya msingi Ilola iliyopo katika kata ya Ilola tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga.
Walioshuhudia tukio hilo walisema mwanafunzi huyo aliyekuwa anasoma darasa la tano alifariki dunia baada ya kupigwa makofi na ngumi sehemu za kichwani na mwanafunzi mwenzake aitwaye Sophia Mathew(12) ambaye pia ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo kutokana na ugomvi uliotokana na kugombania daftari.
Akizungumza na Malunde1 blog, afisa mtendaji wa kata ya Ilola Mahona Joseph alisema tukio hilo lilitokea wakati wanafunzi hao wakigombania daftari ambapo marehemu alikuwa ameng’ang’ania daftari aliloazima kwa mwanafunzi mwenzake Sophia Mathew kwa ajili ya kuandika dondoo za daftari hilo.
Alisema kitendo cha kung’ang’ania daftari hilo wakati siyo mali yake kilimkera mwanafunzi mwenzake na kuzua ugomvi kati ya wanafunzi hao na kubababisha kifo cha mwanafunzi huyo.
Naye mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ilola Magere Jonas aliiambia malunde1 blog kuwa tukio hilo lilitokea wakati wanafunzi hao wakigombana darasani na kwamba huenda mwanafunzi huyo aliumia kisogoni baada ya kuanguka wakati wa ugomvi huo.
“Ilikuwa muda wa saa saba mchana wakati wanafunzi wengi wameenda kula wengine wakiwa bado wako shuleni,walimu walikuwa majumbani lakini mimi na mwalimu mkuu msaidizi tulikuwa chini ya mti tunapunga upepo,mara akaja mwanafunzi mmoja akasema kuna wanafunzi wanagombana darasani, ndipo tukaenda na kumkuta amelala chali darasani” alisimulia mwalimu mkuu.
“Kufuatia hali hiyo tukachukua jukumu la kumpeleka kwenye zahanati ya Ilola ambapo nesi akatushauri kwenda kituo cha afya cha Bugisi kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo mwanafunzi huyo lakini tulipofika Bugisi tukaambiwa tayari ameshafariki dunia,tunahisi pengine aliumia kisogoni”,alieleza mwalimu Jonas.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Longinus Tibishubwamu alisema wanamshikilia mtuhumiwa Sophia Mathew anayedaiwa kumpiga Veronica Venance sehemu za kichwani kwa kutumia mikono yake.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment