Habari zilizopatikana jana mjini Songea na kuthibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Februari 17 mwaka huu majira ya saa nane mchana katika eneo la Lizaboni mjini Songea ambako Anitha Kasimu Mbawala(40)mkazi wa kata ya Ruvuma mjini Songea yalifanyika mazungumzo ya kutaka kumuuza kwa mfanyabiashara huyo.
Akifafanua zaidi kamanda wa polisi kuwa inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio Sophia alimfuata mtu mmoja ambaye jina lake linaendelea kuhifadhiwa kwa sababu za kiusalama na kumuambia kuwa ili aweze kufanikiwa katika biashara zake inabidi afanye zindiko kwa kutumia maiti ya binadamu.
Alieleza zaidi kuwa Sophia alimuambia mtu huyo kuwa kwa sasa wafanye biashara kati yake na mfanyabiashara huyo kwa sababu yeye ana mama yake mdogo aliyemtaja kuwa ni Anitha ambaye alikuwa na ugomvi nae hivyo ampatie kiasi cha shilingi milioni kumi ili akamuuwe na amletee maiti ya mama huyo ikiwa imehifadhiwa kwenye gunia.
Kamanda Msikhela aliendelea kufafanua kuwa inadaiwa mfanyabiashara huyo alikataa kuletewa maiti na badala yake alimueleza Sophia kuwa aletewe mtu mzima au akiwa hai na akamuambia kuwa atamuua yeye mwenyewe ila Sophia amlete mama yake mdogo akiwa mzima na kuwa alimuomba Sophia ampunguzie bei badala ya shilingi milioni kumi amuuzie kwa shilingi milioni 6.5.
Alisema kuwa baada ya kukubaliana mfanyabiashara huyo alitoaq taarifa kwa jeshi la polisi juu ya tukio hilo na askari polisi wakiwemo askari kanzu kutoka ofisi ya Afisa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Ruvuma ambao waliweka mtego wa kuhakikisha kuwa wanamnasa Sophia.
Alisema kuwa Februari 18 mwaka huu majira ya asubuhi Sophia alikwenda Ruvuma kumfuata mama yake mdogo kwa kumdanganya kuwa kuna mwanaume amempenda mama yake alikataa ndipo Sophia alipomrubuni tena na kumueleza kuwa kuna matajiri wanataka mtu wa kumuajiri ndipo Anitha alipokubali na kupelekwa mpaka Lizaboni katika eneo walilokuwa wamepanga kukutana mnunuzi waliekubaliana siku ya nyuma yake.
Alisema kuwa inadaiwa kuwa ilipofika majira ya saa 5;30 katika eneo hilo la Lizaboni askari polisi walifanikiwa kumkamata Sophia akiwa na mama yake mdogo tayari kwa kumuuza na kabla yake mfanyabiashara huyo alikuwa amekwenda benki kuchukua fedha kwa ajili ya kumlipa Sophia ndipo polisi walipomkamata.
Hata hivyo kamanda Msikhela alisema upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.
Na Gideon Mwakanosya- Jamvilahabari.com Songea
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment