Dhana ya kuwa matajiri hawapati usingizi mzuri au kuwa maskini walijaaliwa usingizi mnono umefutiliwa mbali kulingana na utafiti mpya.
Kulingana na ripoti ya utafiti iliyochapishwa katika jarida la Pediatrics, matajiri hupata usingizi bora zaidi ikilinganishwa na wenzao kutoka jamii za wastani na masikini.
Utafiti huo uliofanywa katika shule za serikali na za kibinafsi nchini Marekani katika kipindi cha kati ya mwaka wa 1991 na 2012 ulihusisha wanafunzi 270,000. Matokeo ya utafiti huo yalibaini kuwa vijana waliotoka katika familia za kitajiri walikuwa wakilala kwa masaa mengi zaidi ikilinganishwa na wale waliotoka katika familia maskini.
Ripoti hiyo pia ilisema kuwa wanaume walikuwa wakipata usingizi bora ikilinganishwa nawanawake huku vijana wenye ngozi nyeupe nchini humo wakipata usingizi bora ikilinganishwa na wale wenye ngozi nyeusi na wale kutoka familia za wahamiaji.
Utafiti huo ulionyesha kuwa utumiaji wa madawa ya kulevya, matatizo shuleni, matatizo ya kiakili na kuongezeka kwa uzito wa mwili kama sababu zilizopelekea kupunguwa kwa ubora wa usingizi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment