Mwigizaji wafilamu anaesifika kwa uwezo wake mkubwa wakuvaa uhusika anapokuwa anaigiza, Riyama Ally amelezea furaha yake ya kuwa mama na kuwatakia baraka wanawake na wakina mama wote.
“Raha ya dunia ni watoto tajiri na maliyake maskini na wanawe tupende watoto wote kwani watoto ni zawadi toka kwa MUNGU pia watoto ni faraja kubwa sana.... Asante sana MUNGU kwa zawadi ya Fatma Nakupenda sanaaaaaaaaaa Fatma kwani umenipa faraja ya kuitwa mama nawaombea wanawake wote waliokua bado hawaja jaaliwa kupata watoto basi inshallah Mwenyezimungu akawajaalie kizazi chema kizazi bora inshallah amin.
Na kwa walio fiwa na watoto wao Allah awajalie subira na faraja za nafsi awajalie watoto wingine inshallah awe watoto wa kheri amin Nawapenda sanaaaaaaaaaa".- Riyama aliandika haya mtandaoni.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment