MTANGAZAJI maarufu wa Runinga, Maimartha Jesse hivi karibuni aliamua kumtolea uvivu, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ kwa kumpa kitchen party ya nguvu.
Akichonga na Centre Spread, Mai alisema kuwa anachoumia ni kwamba kila mtu mjini hapa anamsema Lulu vibaya wakati yeye alikuwa ni rafiki yake wa karibu.
“Kama atalia na alie, kama atacheka na acheke lakini nimeshachoka na mambo yake kwa sababu yeye ni umiza kichwa, anasumbua vichwa vya watu kwa matendo yake,” alisema Mai.
Aidha, Mai alisema anamsema Lulu kama mdogo wake na mtu aliyemfanya akapata jina mjini hapa kuwa aache tabia ya kulalala gesti na kuwa karibu na wanaume wasio riziki.
Post a Comment
Post a Comment