
Mwanamziki Madonna akiwa ameanguka jukwaani katika tuzo za Brits
Mwanamuziki nguli, Lady Madonna jana alimalizia
vibaya shoo yake nzuri ya kukumbukwa baada ya kuanguka kwenye ngazi jukwaani,
kufuatia kusukumwa na dansa wake wakati akitumbuiza katika tuzo za Uingereza
'BRIT Awards 2015'. Wakati akimalizia malizia kuimba wimbo Living For Love,
ghafla Madonna akashindwa kuikusanya miguu yake na kuporomoka chini wakati
akipishana na dansa wake katika ngazi za jukwaa la ukumbia wa London's 02
Arena. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 56 alishituka baada ya kuanguka na
kuacha kuimba kwa muda, lakini akajikusanya kusanya na kuinuka kisha kuendelea
na shoo yake hadi mwisho.

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment