Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mrembo na mwigizaji wa filamu, Wema Sepetu amefunguka na kudai kuwa mwigizaji Van Vicker wa Ghana, alichania kwa kiasi flani, kupelekea aachane na aliekuwa mpenzi wake, Diamond.
Kwamujibu wa GPL,akizungumzia sababu za kumwagana na Diamond, alisema pamoja na sababu nyingine, Van Vicker alihusika kuwafanya wamwagane na mpenzi wake huyo waliyedumu kwenye penzi zito lililokuwa gumzo kila kona ya Bongo.
“Kuna vitu vingi vimechangia lakini Van pia amechangia, alianza ku-like picha zangu, nikamwambia Dai (Diamond), akaniambia achana naye, baadaye tulibadilishana namba, tukawa tunawasiliana.
“Ilipofika wakati amenitaka tufanye kazi pamoja, nilipomwambia Diamond ndiyo matatizo yalipoanzia hadi kufikia hatua ya kuachana,” aliweka nukta Wema.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
01 Jan 2015

Post a Comment

 
Top