Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu jijini Dar es salaam nchini Tanzania imetoa tahadhari kwa wananchi juu ya kuwepo kwa baadhi ya watu ambao ni matapeli na wanatumia vibaya jina la ikulu kwa kusema kwamba kuna nafasi za ajira na wana uwezo wa kuwapatia ajira kwa kutoa fedha.
  
Tahadhari hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu Bw. Salva Rweyemamu wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia kutokea kwa matukio kadhaa ya mfululizo ya watu kutapeliwa kwa kutafutiwa kazi ikulu.
  
Aidha Salva amesema Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kufanya maamuzi ya watuhumiwa wa kashfa ya Tegeta Escrow ambao walikuwa wakifanyiwa uchunguzi kama alivyoahidi wakati wa mkutano wake na wazee wa mkoa wa Dar es salaam tarehe 22 mwezi Disemba mwaka jana.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top