Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
ronaldo 
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ametwaa tuzo nyingine katika kipindi cha siku tatu zilizopita baada ya kutajwa kuwa mchezaji bora wa muda wote kwenye historia ya soka la Ureno .
Ronaldo ametwaa tuzo hiyo katika hafla maalum iliyoandaliwa kwenye Gala  Quinas De Ouro iliyofanyika huko Ureno ikiwa imeandaliwa kutoa tuzo za heshima kwa wanasoka mbalimbali wa Ureno ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 ya shirikisho la soka la ureno.
Ronaldo ametwaa tuzo hiyo akiwa amepigiwa kura nyingi kuliko magwiji wa soka wa Ureno akiwemo Luis Figo na hayati Euesebio ambaye alifariki dunia mwaka jana baada ya kuugua maradhi ya kiharusi kwa muda mrefu .
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikuwepo kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za Quinas de Ouro nchini Ureno.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikuwepo kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za Quinas de Ouro nchini Ureno.
Ronaldo ametwaa tuzo hiyo baada ya mafanikio aliyoyapata hasa akiwa na klabu ambapo ametwaa mataji karibu yote akiwa na Manchester United na Real Madrid .
Zaidi ya hapo Ronaldo amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara tatu akiwa mreno pekee kutwaa tuzo hiyo mara tatu hali ambayo imechangia kutwaa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa Ureno kwa miaka yote.
Hafla ya utoaji tuzo hizo ilihudhuriwa na marais wa FIFA na UEFA Sepp Blatter na Michel Platinni na Ronaldo hakuweza kuhudhuria tuzo hiyo na ilichukuliwa kwa niaba yake na wakala wake Jorge Mendez.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top