Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Real Madrid, mabingwa mara kumi wa Ulaya, wameweza kushikilia nafasi ya kwanza kama timu tajiri zaidi duniani kwa mwaka wa kumi mfululizo, katika orodha ya Deloitte ya timu tajiri duniani.

Manchester United imesogea hadi nafasi ya pili kutoka ya nne, katika tathmini iliyofanywa kwa kuzingatia mapato ya msimu wa 2013-14.

Bayern Munich, Barcelona na Paris Saint-Germain zimechukua nafasi ya tatu, nne na tano.
Klabu za England za Manchester City, Chelsea, Arsenal na Liverpool zimo katika nafasi kuanzia sita hadi tisa, zote zikionesha ongezeko zuri la mapato.
Orodha kamili ya kumi bora pamoja na mapato msimu wa 2013-14 ni kama ifuatavyo kwa sarafu ya Euro:
(Kwenye mabano ni mapato ya msimu wa 2012-13)
•1. Real Madrid: 549.5m (518.9m)
• 2. Man Utd: 518m (423.8m)
• 3. Bayern Munich: 487.5m (431.2m)
• 4. Barcelona: 484.6m (482.6m)
• 5. Paris Saint Germain; 474.2m (398.8m)
• 6. Manchester City: 414.4m (316.2m)
• 7. Chelsea: 387.9m (303.4m)
• 8. Arsenal: 359.3m (284.3)
• 9. Liverpool: 305.9m (240.6m)
• 10. Juventus: 279.4m (272.4m)

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top