March 19, 2025 10:52:06 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Azam 1
Simba sasa imeamka kwenye Kombe la Mapinduzi baada ya kufanikiwa kutinga nusu fainai ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kuichabanga Taifa ya  Jang'ombe kwa mabao 4-0.




Simba imeonyesha inaweza baada ya kuzitumia dakika 45 za kipindi cha pili kwa kuichapa Taifa mabao yote manne kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Shujaa wa Simba leo ni Ibrahim Ajib aliyefunga mabao matatu, hat trick na kufanikiwa kuondoka na mpira wa zawadi wakati mkongwe Shabani Kisiga alimalizia bao la nne.

Simba ilitawala mpira tokea kipindi cha kwanza, lakini Taifa walitoa upinzani mkubwa na kufanya wamalize mpira wakiwa sare ya bila bao hadi mwisho wa kipindi cha kwanza.

Nyota wa mchezo huo alikuwa ni beki mpya wa Simba, Ramadhani Kessy ambaye aliondoka na zawadi ya king'amuzi ya king'amuzi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
07 Jan 2015

Post a Comment

 
Top