Juzi Mambo yalikuwa si Mambo katikati ya Jiji la Dar baada ya Vijana Wanaojiita Panya Road Kufanya Fujo Mitaa ya Sinza, Magomeni na Mwananyamala , Mmoja wa wahanga wa Fujo hizi ni Mwanamuziki Ray c..
Hichi Ndicho Kilichomtokea:
"Sina hamu na hawa panya road, jana nilikuwa sehemu flani sinza nakula kitimoto nilivyoona watu wanakimbia nikatoka nduki bila viatu nikaingia kwenye gari mbio mara mbele yangu nikakutana na lundo la watu wakinoa mapanga barabarani, niligeuza gari utafikiri niko kwenye movie nikajikuta nimefika osterbay polisi bila viatu mpaka askari wakanicheka! !!!!!!!!!!Serikali tunaomba mkamate hawa vijana kwakweli maana tumezoea amani sasa mambo kama haya yakitokea yanakosesha amani kabisa kwa wananchi!Na uhakika Jeshi la polisi litafanya kazi yake yani nilijihisi kama niko Rwanda maana nakumbuka mapanga yale niliwahi yaona kwenye muvi ya Somewhere in April na Hotel Rwanda!!!!Sasa wale waliosema bora damu imwagike nadhani kauli itabadilika maana kama Panya Road wanatupelekesha hivi je hiyo Vita!!!, Je hiyo vita, si tutapanda juu ya nyumba zetu!!!!! Jamani msicheze na haya mambo jamani, amani ndio sifa kuu ya nchi yetu........Eeh Mungu tuepushe na haya mambo....." Ray C
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment