Asilimia kubwa ya mastar wengi wa duniani huwa wanapenda kutengeneza kitu ambacho kitakua tofauti na wengine ili kumtengenezea utambulisho wake popote anapokuwepo.
Tumeona style kadhaa za mavazi ambayo yanapovaliwa na mastar huwa yanachukua chart kwa kuvaliwa pia na watu wa kawaida ambao huwa wanavutiwa nayo.
Kingine ni style ya nywele ambazo mastar wamekuja nazo ikiwemo kiduku ambapo kwa sasa mastar wengi wananyoa hivyo,kuna wengine wanaachia nywele zinakua nyingi style hii wengi wao huita ‘Mwembe’ kwa wingi wa nywele kichwani.
Star kutoka kundi la Original Komed Joti yeye mwaka 2015 kaamua kuja na style hii ambayo hajasema inaitwaje ambapo kwenye ukurasa wake wa Instagram alipost picha akiwa ananyoa na alipomaliza.
Katika post yake ya kwanza aliandika>>’Kwaheri 2014′ hii alionekana akinyoa na katika post nyingine aliandika>>’Now karibu 2015,karibu babaaa…..my new style’.
Credit Millardayo
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment