Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Liverpool-v-Olympiacos-Steven-Gerrard-Testimonial
Zikiwa zimepita saa 24 tangu nahodha wa zamani wa England Steven Gerrard atangaze kuwa ataachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, wengi waliozipata hizo taarifa walikua na hamu ya kujua mkali huyu ataelekea wapi?

Taarifa hii inakuja kama uthibitisho wa tetesi ambazo zilisikika tangu awali kwamba Gerrard angesajiliwa na timu inayoshiriki ligi ya Marekani maarufu kama MLS kama ambavyo imekuwa kawaida kwa nyota kadhaa ambao hukaribia kumaliza nyakati zao za kucheza soka la ushindani Ulaya.
Timu ambayo imetajwa sana kuwa na nia ya kumsajili Gerard ni Los Angeles Galaxy ambayo ni moja ya klabu maarufu kuliko zote kwenye ligi ya Marekani.
Los Angeles Galaxy imetajwa kuwa mbioni kumsajili Steven Gerard.
Los Angeles Galaxy imetajwa kuwa mbioni kumsajili Steven Gerard.
Umaarufu wa Galaxy uliongezeka maarufu wakati klabu hiyo ilipomsajili nyota wa zamani wa Manchester United David Beckham wakati alipomaliza mkataba wake na Real Madrid.
Hakuna ubishi kuwa Becks aliiongezea umaarufu ligi ya Marekani hali ambayo imechangia kuwavuta nyota wengine kusajiliwa na timu kadhaa za ligi hiyo.
Steven Gerard siku ya ijumaa alitangaza kuwa ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top