Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MKAZI wa Dodoma, Ramadhan Zuber ambaye alikuwa abiria kwenye basi la Champion amefariki dunia akiwa safarini.

Akizungumza na Mpekuzi mjini Kibaha, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema kuwa Zuber (29) alikuwa akisafiri toka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 16, saa 3:30 asubuhi katika kijiji cha chamakweza wilaya ya Bagamoyo ambapo alibainika kuwa ameshafariki dunia.

Alisema kuwa Zuber alikuwa amekaa kiti namba 3 kwenye basi hilo lenye namba za usajili T 909 BRA.

Chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika. Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Tumbi kwa ajili ya uchunguzi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top