Shangwe Thani, Shinyanga
UKATILI! Mwanamke mmoja, Regina Salago (24) (pichani) ameuawa kinyama kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kuvunjwavunjwa shingo na mikono na mume wake, Kishimba Keya, kutokana na wivu wa kimapenzi.
UKATILI! Mwanamke mmoja, Regina Salago (24) (pichani) ameuawa kinyama kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kuvunjwavunjwa shingo na mikono na mume wake, Kishimba Keya, kutokana na wivu wa kimapenzi.
Regina Salago enzi za uhai wake.
Tukio hilo la kinyama, limetokea hivi karibuni katika Kijiji cha
Maganzo, Kata ya Songwa wilayani Kishapu, Shinyanga.Akizungumza na
gazeti hili kuhusu tukio hilo, mama mzazi wa Regina aliyejitambulisha
kwa jina la Catherine Kondo (45) alisema siku mbili kabla ya kifo, binti
yake huyo alikuwa amerudi nyumbani kutoka kwa mumewe kwa nia ya
kuachana naye.
‘’Siku aliyorudi mwanangu aliniambia amechoshwa na vitendo vya wivu
wa kupita kiasi anavyofanyiwa na mume wake, ameona bora arudi nyumbani
aanze upya maisha akiwa huru hata kama ni ya shida,’’ alisema mama huyo.
Aliongeza kuwa Regina alishinda siku mbili tu nyumbani hapo ndipo
mume wake alimfuata na kumbembeleza kuwa waondoe tofauti zao na kwamba
alikuwa amejirekebisha.
“Regina alikataa katakata kurudi kwa mwanaume huyo kutokana na
vitendo vya kikatili na unyanyasaji alivyokuwa akifanyiwa kiasi cha
kukosekana kwa amani kwa kusingiziwa alikuwa akitembea nje ya ndoa yao,”
alisema Catherine.
Kufuatia hali hiyo mwanaume aliamua kubadili msimamo na kumpa
shilingi 40,000 Regina kama kumuomba msamaha akashawika kuondoka naye
kurudi kwao.Habari zinadai walipofika kwao alimshambulia kwa kumpiga na
springi ya gari na kuivunja mikono na shingo kwa kutumia chuma hicho
kizito.
Baada ya kumuua, Kishimba alimpigia simu mama mkwe wake mara kadhaa
akimhimiza aende nyumbani haraka kwa kuwa mtoto wake Monica (mdogo wa
Regina) alikuwa mgonjwa mahututi.Aliporudi nyumbani alianza kumtafuta
Regina na alipokwenda kwa mumewe alimkuta akiwa amelala kifudifudi na
damu ikiwa imetapakaa mwili mzima, akiwa amekata roho.
Mama huyo aliongeza kuwa, kufuatia tukio hilo alipiga mayowe ya
kuomba msaada kwa majirani na baadaye polisi waliitwa eneo la tukio.Mama
huyo alisema kuwa muuaji alifanikiwa kutoroka na kuwaacha watoto wake
wawili, Frank (5) na Minza (3) aliozaa na marehemu.
Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, SACP Justus Kumugisha
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. “Sasa hivi tunamtafuta muuaji ili
aweze kufikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Kamugisha.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment