Simba rasmi imemfungashia virago kocha wake Patrick Phiri na nafasi yake inachukuliwa na Goran Kopunovic raia wa Serbia.
Kopunovic anaingia kwenye rekodi ya Waserbia waliowahi kuifundisha Simba akiwemo Milovan Cirkovic.
Taarifa za ndani ya Simba zinaeleza Mserbia anatarajia kuwasili nchini Jumatano na Phiri ame

ishapewa taarifa hiyo.
Kuponovic aliwahi kuinoa Polisi Rwanda kwa mafanikio makubwa na kuiwezesha kuwa tishio mbele ya vigogo APR na Rayon.

Nafasi ya Kocha ya Msaidizi, kuna taarifa Simba ilifanya mazungumza na na Jean Marie raia wa Rwanda aliyewahi kuipa Atraco na Rayon ubingwa wa Rwanda kwa nyakati tofauti.
Lakini hata hivyo inaonekana wameshindwa kuelewana na Selemani Matola anaendelea kuitumikia.
Kauli ya phiri baada ya kutimuliwa
Kocha Patrick Phiri amesema ametaarifiwa kuhusiana na kibarua chake kusitishwa.
Phiri raia wa Zambia amesema ni suala la kawaida kumtokea kocha, hivyo hana kinyongo na uongozi wa klabu hiyo.
"Wamenitaarifu kuhusiana na kuachishwa kazi, hili si jambo jipya, ingawa niliona tungeweza kubadilisha mambo.
"Najua Simba wanataka kufanya vizuri, hivyo siwezi kumlaumu mtu na utaona mwendo wa timu yetu ulivyokuwa," alisema Phiri.
Phiri amesema anasubiri kiasi cha fedha alichokuwa anadai ambacho hakueleza ni kiasi gani, halafu ataanza safari ya kurejea kwao Zambia.
"Nikimalizana nao kuhusiana na malipo yangu, nitajua lini ninakwenda nyumbani," alisema Phiri.

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment