MWANANCHI
Serikali ya Qatar imesema iko tayari kuajiri Watanzania katika nyanja mbalimbali zakitaaluma kwa kuwa Taifa hilo lina uhaba wa wataalam katika maeneo mengi.
Hayo yako katika mazungumzo yaliyofanyika jana kati ya Waziri mkuu Mizengo Pinda na Waziri mkuu wa Qatar Sheikh Abdullah Nasser Al Thani ofisini kwake mjini Doha.
Akizungumza mara baada ya mkutano huo Waziri Mkuu alisema Serikali ya Qatar imesema ipo tayari kuwapa Watanzania ajira katika maeneo mbalimbali na kuna baadhi ya Watanzania tayari wameshaingia kwenye soko la ajira la Qatar lakini idadi haitoshi kutokana na ukweli kwamba nchini humo kuna kazi nyingi.
Pinda jana alitarajiwa kuwa na mazungumzo na Naibu Waziri wa madini,Waziri wa Uchumi na Waziri wa miundombinu na usafirishaji na Waziri wa kazi na maendeleo ya jamii.
MWANANCHI
Ama kweli haya maajabu,Wapigakura wa Wilayaya Ilemela jana walipigwa na butwaa baada ya kufika kituo cha kupiga kura na kukuta mgombea wa nafasi ya Uenyekiti kupitia CCM ameshatangazwa mshindi.
Tukio hilo lilisababisha wafuasi wa Chadema waliofurika kwenye kituo hicho kupinga matokeo hayo jambo lililowafanya polisi wawatawanye kwa mabomu ya machozi.
“Haiwezekani watuwamejitokeza kupiga kura alafu wanakuta matokeo tayari yamebandikwa…ni jambo la ajabu na la kushangaza watu hawajapiga kura,matokeo yametangazwa,lazima suala hilo litolewe ufafanuzi wa kina”alisema Mbunge wa Ilemeka Highness Kiwia huku akimsimika Ramadhan Said kutoka Chadema kuwa Mwenyekiti wa mtaa huo.
Hata hivyo msimamizi wa uchaguzi huo Wilaya ya Ilemela Justin Lukaza alisema matokeo hayo ni sahihi,kwani uchaguzi huo ulifanyika Desemba 14 lakini wakashindwa kutangaza matokeo kutokana na sababu zlizojitokeza.
MWANANCHI
Wanafunzi 344 waliomaliza darasa la saba mwaka huu Mkoani Arusha wamebainika kuwa hawajui kusoma,kuandika wala kuhesabu.
Afisa elimu Mkoa wa Arusha Nestory Mloka alitoa taarifa hiyo juzi katika kikao cha elimu kilichoketi juzi kwa ajili ya kuchambua matokeo ya darasa la saba na kuwapangia shule wahitimu waliofaulu mitihani.
Mloka alisema kati ya wanafunzi hao 334 waliomaliza darsa la saba bila kujua kusoma na kuandika wavulana walikua 163 na wasichana walikua 181.
Alisema Wilaya ya Ngorongoro ndiyo inayoongoza kuliko sehemu nyingine yoyote Arusha kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi ‘vilaza’ wanaofikia 230.
Alisema wanafunzi waliomaliza darasa la saba ni ni kati ya wanafunzi 34,348 waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu Mkoani Arusha.
MTANZANIA
Hali ya tafrani ilizuka jana jijini Dar es salaam baina ya Katibu mkuu wa Chadema Wibroad Slaa na askari wa jeshi la Polisi ba ada ya askari kumhoji kiongozi huyo hatua yake ya kufanya mkutano bila kibali.
Tafrani hiyo ambayo iliibuka eneo la Tegeta Gereji ilianza majira ya saa 11.50 jioni baada ya kiongozi huyo kuwasili na kuanza kuhutubia ambapo wananchi walikua wakitoa malalamiko yao dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana kwa kumilikisha eneo hilo kwa mwekezaji.
Baada ya wananchi kuwasilisha matatizo yao Dk Slaa alisema kwa muda mrefu Watanzania wamekua wakitenganishwa na vyama ila linapotokea suala lenye maslahi kwa Taifa huwa wanaondoa itikadi zao.
“Haiwezekani Serikali iwakabidhi eneo halafu leo iwaondoe..ni jambo ambalo halikubaliki kwani mwekezaji mmoja hawezi kuwa na manufaa kushinda watu 4000.
MTANZANIA
Wazabuni waliopewa tenda ya kulisha Jeshi la Polisi na vikosi vyake nchini wamelalamikia hatua ya ofisi ya uhasibu Polisi makao makuu kushindwa kuwalipa deni la zaidi ya milioni 700 wanazodai tangu mwaka 2008.
Pamoja na hali hiyo wamepinga hatua ya mhasibu mkuu wa Jeshi hilo Frank Msacky ya kufanya malipo kwa upendeleo na hata kumtuhumu amekua akificha nyaraka za kumbukumbu za malipo za wazabuni hao.
Wazabuni hao walisema hatua ya kushindwa kulipwa inakwenda kinyume na kauli iliyotolewa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya ya kulipa madeni yote ya nyuma.
Walisema kwa muda mrefu wamekua wakisotea malipo yao ambayo yamekwamishwa na idara hiyo ya uhasibu.
“Madeni yetu tunadai tangu 2008 na CAG aliainisha tulipwe…je inakuaje vocha za malipo zimeandaliwa lakini hatulipwi?walisisitizaWazabuni .
NIPASHE
Chama cha Wananchi CUF Wilayani Lindi kinajiandaa kumfikisha mahakamani Mke wa Rais Mama Salma Kiwete ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoani humo kwa maelezo ya kutumia rasilimali za Serikali kinyume na Sheria.
Mwenyekiti wa CUF Salum Bar’wan aliwaambia waandishi wa habari kuwa rasilimali zinazotumika bila kufuata sheria ni magari ya Serikali na watendaji wake wakiwemo wakuu wa Idara mbalimbali kama mkuu wa Polisi Wilaya OCD na Mkurugenzi wa Manispaa.
“Tumeshuhudia misafara yake ya kampeni ya uchaguzi wa Serikali za mitaa huku akiongozana na watendaji wa Idara mbalimbali za Serikali akiwemo OCD na Mkurugenzi wa Manispaa na watendaji wa Idara mbalimbali kinyume na kanuni”alisema.
Alisema kitendo kilichofanywa na Mama Salma cha kutumia mali za Serikali ni kinyume na utaratibu na wamewasiliana na mwanaseheria kuona utaratibu wa kuandaa mashtaka dhidi ya Mjumbe huyo wa NEC.
Credit Millardayo
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment