Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
torres
Siku za Fernando Torres kutambulishwa kama mshambuliaji wa Ac Milan na Chelsea zinazidi kukaribia kufikia mwisho baada ya usajili wa mchezaji huyo ndani ya timu yake ya zamani ya Atletico Madrid kukamilika .
Tayari makubaliano baina ya pande zote zinazohusika yamefikiwa na kilichobaki na kwa mikataba rasmi kutiwa saini na inatarajiwa kuwa mpaka kufikia tarehe 30 ya mwezi huu Torres ataanza kufanya mazoezi na kikosi cha Diego Simeone.
Chelsea imekubali kumruhusu Torres kuondoka bure.
Chelsea imekubali kumruhusu Torres kuondoka bure.
Usajili wa Torres ulianza kuiva baada ya klabu inayommiliki ya Chelsea kukubali kumruhusu mchezaji kuondoka bure hali iliyomfanya awe mchezaji kamili wa Ac Milanambayo kwa upande wake ilikubali kumbadili na mshambuliaji wa kimataifa wa Italia, Alesio Cerci ambaye anacheza Atletico Madrid.
Fernando Torres alicheza kwa kiwango cha juu akiwa na Liverpool lakini mambo yalianza kumwendea kombo baada ya kuondoka kwenye klabu hiyo .
Fernando Torres alicheza kwa kiwango cha juu akiwa na Liverpoollakini mambo yalianza kumwendea kombo baada ya kuondoka kwenye klabu hiyo .
Habari toka huko nchini Hispania zinasema kuwa wawakilishi wa pande zote zinazohusika kwenye makubaliano haya walikutana siku ya jumamosi na kufanya mazungumzo ambayo yaliashiria makubaliano ya msingi juu ya usajili wa wachezaji hawa wawili (Torres naCerci) na inatarajiwa kuwa mpaka kufikia jumanne (Dec 30) Torres atatambulishwa kuwa mchezaji mpya wa Atletico Madrid.
Torres na kocha wa sasa wa Atletico Madrid Diego Simeone waliwahi kucheza pamoja kwenye klabu hiyo miaka kumi iliyopita .
Torres na kocha wa sasa wa Atletico Madrid, Diego Simeonewaliwahi kucheza pamoja kwenye klabu hiyo miaka kumi iliyopita .
Hii itakuwa mara ya pili kwa Fernando Torres kufanya kazi na Diego Simeone baada ya wawili hawa kuwa pamoja kama wachezaji katika miaka ya 2000 wakati Torresalipokuwa anaanza maisha yake kama mshambuliaji chipukizi kwenye kikosi cha Atletico Madrid.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top