Rose Ndauka amesema kwakuwa mwanae ameshafikisha miezi 9, yupo tayari kurejea kazini baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu kutokana na likizo ya uzazi.

Hivi karibuni Ndauka aliachana na baba wa mwanae, Malick Bandawe aka Chiwaman. Japo Ndauka aliwahi kuiambia Bongo5 kuwa wa walikaa pamoja na kuchagua kuachana kutokana na kuwepo tofauti zisizosuluhusishika, Chiwaman ameiambia EATV kuwa hajui sababu ya kuachana kwao.
“Mimi sina sababu yoyote labda yeye anaweza akawaambia sababu,” alisema.
Wawili hao walikuwa na mipango ya kufunga ndoa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment