Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Tumekuwa tukipata taarifa zinazohusu matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara nchini Tanzania, hali ambayo imeonekana kukithiri katika siku za usoni huku jeshi la polisi likitoa ahadi ya kufanya jitihada za kuhakikisha linawatia nguvuni wahusika wa matukio hayo.



Taarifa iliyonifikia  Radio One  inahusu kuuawa kwa mtuhumiwa namba moja wa kesi ya ulipuaji mabomu jijini Arusha, Yahaya Hassan Omar kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi wakati alipojaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi.

Akitoa taarifa za kifo cha mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi wa mkoa wa arusha Lebaratus Sabas amesema marehemu yahaya hassan omari hela maarufu kwa jina la (sensei) ambaye alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu mtuhumiwa huyo alikamatwa wiki mbili zilizopita mkoani morogroro na kupelekwa arusha na bado alikuwa anaendelea kuhojiwa.

Kwa mujibu wa kamandaa sabas mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa marehemu yahaya, alikiri kuwa yeye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa matukio yote ya milipuko ya mabomu na ya kumwagia viongozi wa dini tindikali yaliyowahi kutokea mkoani arusha na maeneo mengine.


Aidha kamanda Sabas Amefaanua kuwa baada ya marehemu ambaye ni mtuhumiwa kukiri tuhuma hizo alikuwa bado anaendelea kutoa ushirikiano kwa kuanza kuonyesha vitendea kazi yakiwemo mabomu ambayo alidaiwa kuyaficha kondoa mkoani Dodoma.




Amesema wakati anasafirishwa walipofika eneo la kisongo katika barabara kuu inayoenda dodoma majira ya usiku alifanya jaribio la kutaka kutoroka na ndipo akapigwa risasi iliyomjeruhi mguu na kiuno na akafariki wakati anapelekwa hosipitali.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top