LICHA ya kutothibitishwa juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa ndoa yake na mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Jide’, mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash ‘Kepteini’ amenaswa na kabinti akiwa kwenye pozi tata za kimahaba hivyo baadhi ya watu kuhoji anasaliti ndoa?
Tukio hilo lililojaa viulizo kibao bila majibu lilijiri Jumatano iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco uliopo Oysterbay jijini Dar kulipokuwa tamasha la wazi la kuibua vipaji vya wasaniii mbalimbali.
Awali, vijana mbalimbali walipanda katika onesho hilo na kuonesha vipaji huku binti huyo jina halikupatikana mara moja, alionekana na rafiki yake ambapo wote walikuwa ni washiriki katika onesho hilo.
~Global Publishers
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment