MCHUNGAJI anayejiita nabii na mtume, raia wa Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyetajwa kwa jina moja la Emmanuel
amejikuta ndani ya majanga kufuatia madai mazito kwamba amemtorosha mke
wa mtu ambaye ni mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa
kasi, Janet Mrema.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mchungaji huyo alifika nyumbani kwa
Jonas Mrema, mume wa Janet, maeneo ya Tegeta-Nyaishozi jijini Dar na
kuishi kama mtumishi wa Mungu lakini polepole alianza mazoea tata na
Janet.
“Kwa sasa tangu tukio hilo litokee ni miezi kama mitatu. Mume
alihangaika sana kumtafuta mkewe hadi jana (Jumatatu iliyopita) ndipo
akampata wakiwa na mchungaji huyo kwenye nyumba moja ambako walikuwa
wakiishi pamoja,” kilisema chanzo chetu.
Iliidaiwa kwamba, mchungaji huyo alipopekuliwa alikutwa na paspoti ya
nchini Burundi wakati yeye ni Mkongo wa Uvira na alionekana kuishi
nchini kinyume na sheria hivyo alifunguliwa jalada la kesi kwenye Kituo
cha Polisi cha Wazo Hili, Tegeta lenye Kumbukumbu Na. WH/RB/7040/2014- KUISHI NCHINI BILA KIBALI.
Juzi, Amani liliwasiliana na Katibu wa Chama cha Waimba Injili
Tanzania, Stela Joel ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema
tayari chama hicho kimemsimamisha uanachana Janet kwa kitendo chake
hicho cha kumtoroka mumewe wa ndoa.
“Ni kweli na Chama cha Waimba Injili Tanzania kimemsimamisha
uanachama Janet. Hatuna mzaha katika maadili,” alisema Stela.Amani
lilimpigia simu mume wa Janet, Jonas Mrema ambapo katika mazungumzo
baada ya salamu alipewa pole kwa matatizo ya mkewe, alisema asante kisha
alipoulizwa kuhusu hali ilivyo aliomba apige simu yeye baadaye kwa vile
alikuwa kikaoni.
Hata hivyo, baada ya saa mbili kupita bila kupiga, Amani lilimpigia
tena simu ambapo iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata
zinaendelea.
Source Gazeti la Amani
Bonyeza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment