Vile vile mvuto zaidi ni ule wa kuona Wabrazil wa Yanga SC, Kiungo Andrey Ferreira Coutinho na Geilson Santos ' Jaja' wakivaana na Simba SC iliyomteka Straika wa Yanga, Mganda Emmanuel Okwi.
Hii itakuwa Mechi ya 4 ya Ligi kwa kila Timu lakini Yanga SC wanaingia wakiwa Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 6 wakati Simba SC wako Nafasi ya 10 wakiwa na Pointi 3.
Msimu huu, Yanga SC walianza kwa kuchapwa 2-0 na Mtibwa Sugar huko Morogoro na kisha kushinda Mechi mbili mfululizo dhidi ya Ruvu JKT na Prisons, zote kwa Bao 2-1 kila moja.
Simba SC wao hawajafungwa lakini hawajashinda hata Mechi moja katika Mechi 3 walizocheza kwa kutoka Sare na 2-2 na Coastal Union na Sare za 1-1 dhidi ya Stand United na Polisi Morogoro.
Refa wa mtanange huu wa Jumamosi ni Israel Nkongo ambae atasaidiwa na Ferdinand Chacha na John Kanyenye wakati Hashim Abdallah atakuwa Refa wa Akiba na Kamishna ni Salum Kikwamba.
Msimu uliopita, Refa Israel Nkongo ndie aliesimamia Mechi ya Mahasimu hawa ambapo Yanga SC waliongoza 3-0 hadi Mapumziko na Simba SC kuweza kurudisha na kupata Sare ya 3-3.
|
Post a Comment
Post a Comment