Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Sabo mwenye umri wa miaka kati ya 30 hadi 34 ameuawa kwa kupigwa mawe na fimbo na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kisha mwili wake kuchomwa moto baada ya kutuhumiwa kuiba ng’ombe wawili katika kijiji cha Shininga kata ya Kilago,tarafa ya Dakama wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha



Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha tukio hilo limetokea jana saa 11 jioni ambapo mwanamme huyo mkazi wa Chibiso alipigwa na wananchi hao baada ya kumtuhumu kaiba ng’ombe wawili mali ya mtu ambaye hakufahamika jina wala makazi yake na thamani ya ng’ombe hao haijulikani.




Kamanda Kamugisha amesema chanzo cha tukio hilo ni wananchi kujichukulia sheria mkononi na kwamba jeshi la polisi linaendelea na msako kuwabaini na kuwakamata wahusika wote wa mauaji hayo.


Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika wa mauaji ha



yo huku akiwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha hasira kali kwani kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria za nchi na haki za binadamu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top