Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
KASHFA! Staa wa filamu za Kibongo, Muhsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ amekanusha tabia ya wasanii wakubwa kuwaomba rushwa ya ngono wasanii chipukizi na kudai wanaziendekeza wao wenyewe.

Staa wa filamu za Kibongo, Muhsein Awadhi ‘Dk. Cheni’.


Akipiga stori na paparazi wetu, Dk. Cheni alisema yeye hajawahi kumuomba msanii rushwa ya ngono, isipokuwa anaamini walio wengi huanzisha mahusiano yaliyo rasmi kwa makubaliano yao kutokana na hisia zinavyowasukuma.
“Sizani kama ni rushwa ya ngono, naamini wengi wanakubaliana, sehemu ya watu wengi mnapokutana inatokea watu kupendana na kuwa wapenzi hilo nakubali sababu ni jambo la kawaida hata wasanii kwa wasanii kupendana, sidhani kama mtu anaweza kulazimishwa kufanya mapenzi ili acheze filamu, mpaka watu kufanya tendo hilo wameshakubaliana,” alisema Dk. Cheni.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top