Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Stori: Andrew Carlos

BAADA ya kuandamwa na skendo kuwa anatoka kimapenzi na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, mkali wa Bongo Fleva, Meninah Abdulkareem ‘Meninah la Divah’ amesema yuko mbioni kumtambulisha mchumba wake.

Meninah Abdulkareem ‘Meninah la Divah’.

Akipiga stori na gazeti hili, Meninah ambaye ni zao kutoka shindano la kuibua vipaji vya kuimba, Bongo Star Search ‘BSS’ 2012 alisema;
“Nimechoshwa kila siku kusikia Diamond, sasa ni bora nimtafute mwanaume yeyote tu kisha nimtambulishe ili ijulikane siko na Diamond,” alisema Meninah ambaye yupo mbioni kuachia ngoma mpya ya Kaniganda.

Meninah Abdulkareem ‘Meninah la Divah’ akipozi.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa Meninah anatoka kimapenzi na Diamond, pia Diamond ameshafika kwao kujaribu kutoa mahari ili amuoe.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
11 Oct 2014

Post a Comment

 
Top