Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MOTO UUONAO HAPO KWENYE PICHA HAPO JUU NI HAO MAJAMBAZI WAKICHOMWA BAADA YA KUUAWA

Wananchi wenye hasira kali wamewaua na kuwachoma moto watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. 

Tukio hilo limetokea leo tarehe 08/10/2014 saa 4:00 Asubuhi katika kitongoji cha NAMANDUNGUTUNGU, maarufu kama MANZESE, kijiji cha SOMANGA, Wilaya ya kilwa Mkoa wa Lindi. 

Watu hao wameuawa ikiwa ni siku moja tu tangu Alipotekwa, kupigwa na kuuawa Mwendesha pikipiki mmoja, maarufu kama bodaboda aliyeulikana kwa Jina la SELEMANI POMBE Mkazi wa Kijiji cha Somanga siku ya Tarehe 06/10/2014 saa mbilin usiku.

 Mwendsha bodaboda huyo alipigwa na kuuawa kisha kunyang`anywa pikpiki yake aina ya SUNLG yenye Namba za usajili T678 CYB.

Tukio hilo limetokea katika eneo la Mitondo kijiji cha Somanga simu.

Mwendesha pikipiki huyo alitekwa na kuuawa alipokuwa anampeleka abiria wake katika kitongoji cha Mitondo na inasemekana abiria huyo alikwenda kukagua mkaa wake. Abiria huyo alifanikiwa kuwatoroka Majambazi hao baada ya kufanikiwa kufungua kamba alizokuwa amefungwa mikononi na miguuni baada ya kumjeruhi vibaya na kumbaka.

  Watuhumiwa hao wa ujambazi wanasadikiwa kuwa ndio wanaofanya uhalifu katika maeneo ya NYAMWAGE-MUHORO-MARENDEGO-SOMANGA, maarufu kama Eneo la Vumbi. Wanateka magari,na kujeruhi watu, kulawiti na kuwanyang`anya fedha na mali zingine kama simu, computer n.k

Mwandishi wa Habari hizi amefanikiwa kupata jina la mmoja aliyeuawa kuwa ni RAMADHANI MAKUNGWA mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa kijiji cha Somanga, na mwingine hatujuweza kupata jina lake lakini kwa taarifa kutoka kwa baadhi ya raia zinasema mtu huyo ni Mwenyeji wa Lindi lakini yupo katika eneo hilo kwa Muda mrefu kidogo.

Kuuawa kwa watu hao kumetokana Na msako mkali ulioendeshwa na wananchi baada ya kukithiri kwa matukio ya ujambazi katika maeneo ya kilwa kama Nangurukuru, Miteja,Kipatimu,Njinjo,na somanga.

 Kwani Mnamo tarehe 03/10/2014 majira ya saa 4:30 usiku, gari zaidi ya kumi zilitekwa na Abiria, madereva na mautingo kuporwa mali na fedha pamoja na baadhi yao kubakwa na kulawitiwa na wengine kujeruhiwa Vibaya. 

Tukio hilo la kusikitisha na kuhuzunisha limetokea katika kijiji cha SNZA-MITEJA.

Baada ya kuwakamata watu hao kabla ya kuwaua, mmoja alisema wasimuue ataonesha ni wapi wenzao watatu walipo pamoja na pikipiki lakini kutokana na hasira za wanachi waliwaua na wengine wamezagaa katika pori la MIBUYU SABA raia aliyetoa taarifa za kuonekana kwa watu hao na kufanikiwa kuwakamata hao wawili aliwaona watu hao.

Hivyo Mpaka wakati huu msako unaendelea, Wananchi wengi wamezagaa na kuzingira pori lote la MIBUYU SABA kuwasaka hao watatu waliosalia pamoja na pikipiki zilizoporwa. 
Kibonajoro.com ndio mtandao wako kwa habari za kitaifa/kimataifa, burudani, michezo, udaku na siasa, Tuwe pamoja huku pia >> Facebook , Twitter

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top